WAKATI
England ikijitayarisha kuivaa Netherlands Jumanne Uwanjani Wembley
Jijini London kwenye Mechi ya Kirafiki ikiwa ni mara tu baada ya
kuwachapa Mabingwa wa Dunia Germany 3-2 Juzi huko Berlin, Meneja wa
England Roy Hodgson amelazimika kumtetea Kepteni wake Wayne Rooney ambae
hayuko kwenye Kikosi hiki kutokana na kuwa majeruhi
Wakicheza bila ya Rooney, Vijana wa England kina Harry Kane, Jamie
Vardy na Eric Dier walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kuipiga Germany Bao
3-2.
Ushindi huo umezua mjadala huko England huku baadhi ya Watu
wakitaka Rooney, ambae ndie Mfungaji Bora katika Historia ya England,
amwagwe kwenye Timu.
Akihojiwa kama moto wa Vijana hao wa England utamfanya ampige chini
Rooney, Hodgson alijibu: "Sifurahishwi ikiwa wakati huu kaumia Watu
wanatajwa kumwagwa kwake. Nina furaha Welbeck amepona na amerejea
vizuri, Kane yuko safi. Nina hakika Wayne akipona tutamtathmini."
Aliongeza: "Yeye ni Kepteni wetu. Ameiongoza Timu vyema kwa Miaka
Miwili sasa na tumeshinda Mechi 10 kati ya 10 katika Kundi letu la EURO
2016. Hastahili kuhojiwa nafasi yake katika Timu!"
KIMATAIFA KIRAFIKI
Jumanne Machi 29
1900 Estonia v Serbia
1900 Montenegro v Belarus
2000 Macedonia v Bulgaria
2030 Greece v Iceland
2100 Georgia v Kazakhstan
2100 Gibraltar v Latvia
2100 Norway v Finland
2115 Luxembourg v Albania
2130 Austria v Turkey
2130 Sweden v Czech Rep
2130 Switzerland v Bosnia-Herzegovina
2145 Belgium v Portugal
2145 Germany v Italy
2145 R. of Ireland v Slovakia
2200 England v Netherlands
2200 France v Russia
2200 Scotland v Denmark
0 comments:
Post a Comment