ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA RTD NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA AFARIKI DUNIA


















Saraha Dumba

 Taarifa zinasema kwamba mkuu wa wilaya ya Njombe Mh. Sarah Dumba amefariki dunia ghafla jana jioni  ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha Habari Kinasema Kwamba Bi, Sarah alikua ofisini hadi mida ya saa tisa jioni ambapo alianza kulalamika kua anajisikia vibaya, akapelekwa katika Hospital ya wilaya Kibena ambapo muda mufupi alifariki dunia.

Akitoa Taarifa za Kifo cha Mkuu wa Wilaya Hiyo , Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi Amesema Marehemu Amefariki Wakati Akiendelea na Matibabu Katika Hospitali ya Mkoa  wa Njombe (Kibena).

Kwa Mujibu wa Dkt.Nchimbi Amesema Kuwa Marehemu Sara Dumba Alifanya Kazi Zake Kama Kawaidi Siku Nzima Hadi na Aliporejea Nyumba  na Kupata Chakula, na Kwamba Mara Baada ya Kupata Chakula Hali Ilibadilika na Kuanza Kutapika Huku Akilalamika Kukosa Hewa Ambapo Alipelekwa Hospitali Majira ya Saa 1:20 na Kufariki Wakati Akipatiwa Matibabu.

Dkt. Nchimbi Amesema Taratibu za Mazishi Bado Zinaendelea na Kwamba Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe Inakutana Leo Asubuhi Kupanga Ratiba Kamili.


 





"Nadhani inaweza kuwa ni tension 
maana tupo kwenye maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji, na yeye amekuwa akishughulika sana na maandalizi hayo ambayo kilele chake ni kesho, sasa leo amefika ofisini kama kawaida, lakini baadaye akasema hajisikii vizuri, baadhi ya kazi akatuma watu, baadaye alikwenda hospitali, lakini muda mfupi baada ya kufika hali ikabadilika, akatapika sana na hapo ndipo alipopoteza maisha" Amesema Dkt Nchimbi.








Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Baadhi Ya Viongozi Wa Dini Waliofika Nyumbani Kwa Marehemu Wamelezea Namna Walivyokuwa Wakishirikiana Na Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba  Wakati Wa Uhai Wake Kwamba Alihimiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji Na Kuwaunganisha Watumishi Wa Mungu Pasipo Kubagua Kanisa.

Kabla ya Kuteuliwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Marehemu Sara Dumba Alikuwa Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania
Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa Wafanyakazi wa Upland's Redio Inatoa Pole Kwa Ndugu, , Jamaa na  Familia ya Marehemu Sara Dumba Pamoja na Uongozi wa Wilaya ya Njombe Hasa Katika Kipindi Hiki cha Majonzi.

Mwili Wa Marehemu Utasafirishwa Siku Ya Kesho Kwenda Jijini Dar es salaam Kwa Mazishi

Mungu Alitoa na Mungu Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe, Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Ma Hali Pema Peponi , Amen






Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment