NJOMBE, Ndoto za kupata maji
kwa wakazi wa kata ya lugenge wialayani njombe zinazidi kufifia baada ya
mhandisi wa maji wa halmashauri ya mji wa Njombe Jobmwakasala kukiri kuwa mradi
wa maji wa lugenge bado ni kitendawili baada ya kuvunja mkataba
Mradi huo umepigiwa
kelele kwa takribani miaka minne sasa bila mafanikio jambo ambalo linaelezwa
kuwa hata mkandarasi aliyeanza kutekeleza mradi huo amegoma kuendelea na kazi
hiyo baada ya kucheleweshewa fedha alizokuwa akidai zaidi ya milioni 300.
Diwani wa kata ya
Lugenge Fileteus mligo amesema kuwa hali iliyofikia ya utekelazi wa mradi huo
inazidi kuwa mbaya kutokana na miundombinu iliyojengwa kama mabomba na mifereji
kuharibika kwa kupanuka zaidi kutokana na mifugo kuendelea kupita humo baada ya
mkandarasi kutelekeza mradi huo.
Mbunge wa jimbo la
Njombe mjini Edward mwalongo amesema hata yeye anashangazwa kuona mambo
hayaendi sawa katika mradi huo ikiwemo miradi mingine ya maji huku akizitupia
lawama idara za manunuzi pamoja na watendaji wa idara ya maji kwamba huenda
ndio chanzo cha kukwamisha miradi hiyo
Job Mwakasala ni
mwandisi wa maji katika halmashauri ya mji Njombe ambaye amekiri kuvunjwa kwa
mkataba na mkandarasi huyo huku jitiohada za kumtafuta mwingine zikiendelea
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uaminifu
Juu ya kutajwa kuwa
huenda watendaji wa idara ya maji na idara ya manunuzi ni chanzo cha kukwamisha
miradi ya maji mwandisi anakanusha tuhuma hizo.
Mradi wa Maji Lugenge
kwa gharama za awali ulipaswa kugharimu kiasi shilingi bilioni 4.7 tangu mwaka
2013 na kutakiwa kukamilika mwaka 2015 ukilenga kuhudumia wakazi wa vijiji vya
Lugenge , Utalingolo , Kisilo pamoja na Kyaula lakini hadi sasa haujakamilika
,.
0 comments:
Post a Comment