Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akikagua madarasa
NJOMBE, Serikali mkoani Njombe imeombwa kujenga nyumba za walimu katika shule mpya ya msingi mpeto iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ili kuwaepusha walimu na adha ya kutembea umbali mrefu hali ambayo imedaiwa kuwa na athari katika utoaji wa taaluma.
Taarifa zinadai walimu
wa shule hiyo hutembea zaidi ya kil 10 kila siku kwenda na kurudi hali ambayo
imedaiwa kuwa na athari katika utoaji wa taaluma.
Shule ya msingi Mpeto
Wakizungumza wamesema mtandao huu wamekuwa wakilipa nauli pamoja na kutumia mishahara yao ili
kuhakikisha wanafika shule na kuitaka serikali kwa kushirikiana na wazazi
kujenga nyumba.
Kutokana na hali hiyo
walimu hao wamesema ni vyema serikali ikaangalia namna ya kufanikisha ujenzi
nyumba na thamani ili waweze kufanya kazi kwa hali.
Mkuu wa mkoa wa njombe
Christopher olesendeka akiwa katika ziara ya kukagua miradi katika wilaya ya
njombe ameugiza uongozi wa wilaya ya Njombe kujenga nyumba hizo za walimu.
Hata hivyo wazazi akiwemo Asheri Mhema wamesema katika kuhakikisha tatizo la umbali linakabiliwa wameamua kujumuika
pamoja kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa shule hiyo yenye madarasa
nane na kuokoa zaidi ya mil 77 zilizokuwa zilipwe kwa mafundi
0 comments:
Post a Comment