Njombe
Kutokana na kukumbwa na changamoto ya umeme wa uhakika katika kiwanda cha kutengeneza misumali na senyenge Rosper company limited mjini makambako Mkoani Njombe , Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri amemuagiza mkurugenzi wa Mji huo kukutana shirika la umeme Tanzania TANESCo ili kuangalia namna ya kitatua tatizo hilo
Bi Msafili ametoa agizo hilo wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha mtu binafsi ikiwa ni maandalizi ya kupokea Mwenge wa Uhuru april 28 mwaka huu huku miradi mingine iliyowekwa mawe ya msingi ikiwa ni mradi wa Nyumba ya mwalimu shule ya msingi ,,,,,,,,,,wenye thamani ya shiringi,,,,,ofisi ya kata ya kitisi, pamoja na mradi wa Nyumba nne za madaktari katika hospital I ya st Joseph ikeru.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri akiweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo katika kata za mji wa Makambako
Fredrick Kazikuboma Afisa utumishi Mji wa makambako amesema katika kuhakikisha Sera ya viwanda inafanikiwa serikali inafanyakila jitihada za kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji wote nchini, hivyo halmashauri itafanya jitihada za kukutana na tanesco kujadili juu ya suala hilo
Nae msimamizi Mkuu wa kiwanda hicho Michael Shirima,amepongeza hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika sekta ya viwanda huku akidai ujio wa Mwenge kiwandani itakuwa nafasi adhimu ya kujitangaza nchi mzima na nje pia.
Msimamizi wa kiwanda cha Rosper Co Limitted Michael Shirima
Mratibu wa Mwenge Halmashauri ya Mji Makambako Taifa Lumato
Ikumbukwe kwamba miradi yote inayowekwa mawe ya msingi hivi sass itapata fursa ya kutembelewa na ugeni Mkubwa utakaokuwepo katika msafara wa Mwenge unaotarajiwa kuingia Mkoani hump mwishoni mwa mwezi April.
Home / Uncategories / TANESCO MKOANI NJOMBE IMEAGIZWA KUANGALIA NAMNA YA KUTATUA TATIZO LA UMEME KATIKA KIWANDA CHA MISUMARI CHA ROSPER CO.LIMITTED KIKLICHOPO MAKAMBAKO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment