Mafunzo hayo
yenye lengo la kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa Umma yamefanyika katika ukumbi wa Milimani Motel Mkoani Njombe
yakifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya
Njombe Bi Ruth Msafili huku yakihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya zote mbili, makatibu
tawala ,Wakurugenzi, Maafisa Utumishi, Makarani wa mikutano pamoja watumishi
wengine.
Miongoni mwa
mafunzo ambayo yametolewa kwa watumishi
hao ni pamoja na Utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi,Sheria za
uendeshaji wa mamlaka za serikali za mitaa,
Muundo ,madaraka na majukumu ya serikali za mitaa, Uendeshaji wa vikao
na mikutano katika mamlaka za serikali za mitaa, Usimamizi na uthibiti wa fedha,
Usimamizi wa Watumishi, Wajibu na Stahiki za Madiwani, Maadili ya Madiwani.
Ikumbukwe kwamba
mradi huu wa PS3 unaofadhiriwa na shirika la USAID unainufaisha mikoa 13 nchi nzima ikiwamo
Njombe , Iringa, Mbeya, Dodoma, Morogoro,
Kigoma, Shinyanga, Kagera, Mwanza, Mara, Lindi Rukwa, Mtwara.
Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Wilaya
, Makatibu Tawala , Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya Njombe, Njombe Mji,
Makambako na Ludewa.
Mkuu wa wilaya ya Njombe BI RUTH
MSAFILI (kulia) ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa mafunzo ( kushoto) ni diwani viti maalumu jimbo la
Njombe Mh ANGELA MWANGENI.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa ADREA TSERE
akiwa katika mafunzo ya uhimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3 ) kwa
waheshimiwa madiwani , wakuu wa wilaya ,Makatibu tawala wa wilaya na matibu
Mratibu wa mafunzo ya
mradi wa kuhimarisha mifumo ya sekta za umma (PS3) uliyofadhiliwa na shirika la
Marekani la USAID DR NAZAR JOSEPH SOLA akiongea
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa waheshimiwa madiwani katika ukumbi wa Mlimani
Mkoani Njombe.
Muwezeshaji wa mafunzo ya
uhimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kutoka chuo cha serikali za mitaa Hombolo
–Dodoma SARAH BENEDICT akitoa mafunzo kuhusu utawala bora na
ushirikishwaji wa wananchi kwa waheshimiwa madiwani pamoja na watumishi wengine
wa serikali waliyohudhulia .
Muwezeshaji wa mafunzo
ya uhimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kutoka chuo serikali za mitaa
Hombolo –Dodoma MANUMBU HEZRONE DAUDI akifundisha kuhusu muundo ,madaraka na
majukumu ya serikali za mita.
Diwani wa viti maalumu kata ya Makambako iliyopo
katika halmashauri ya mji Huo Mh STELLA
UHEMBA akitoa maoni wakati wa mafunzo ya
PS3 .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Ludewa Mh EDWARD LESLIE HAULE akichangia kuhusu uhimarishaji wa vyanzo vya
mapato katika serikali za mitaa.
Waheshimiwa Madiwani pamoja na watumishi wengine kutoka Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa na Makambako.
Waheshimiwa Madiwani na
watumishi wengine kutoka halmashauri ya wilaya ya Njombe pamoja na Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa katika mafunzo.
0 comments:
Post a Comment