WANACHAMA WA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE NJORECU WAKUBARI KULIPWA FIDIA YA MIL 222 NA MUWEKEZAJI WA NJOMBE FILLING STATION
Mwenyekiti wa body ya chama cha ushirika mkoa wa Njombe Clemence Malekela akisoma taarifa wakati wa mkutano mkuu wa wanachama .
==============================
NJOMBE ,Hatimaye muarobaini wa mgogoro wa ardhi baina ya muwekezaji wa Njombe Filling Station na chama cha ushirika mkao wa Njombe NJORECU umefikia hatua nzuri ya usuluhishi baada ya wanachama kupeleka pendekezo la kulipwa fidia ya mil 222 na mwekezaji huyo ili kumaliza mgogoro.
Mgogoro huo wa kipande cha ardhi no 22 kitalu B unadaiwa kusababishwa na mamlaka husika za serikali ambazo zina dhamana ya kutoa hati miliki za ardhi ambapo taarifa zinasema pande zote mbili zina hati halali za umili zilizopata kutoka kwenye ngazi tofauti za mamlaka za serikali.
Wakiongelea jinsi mgogoro huo ambavyo ungeweza kuathiri shughuri za chama cha ushirika endapo ungeendelea wanachama hao wamesema ni pamoja na kutumia muda mwingi mahakani kusikiliza mashtaka sambamba na kutumia pesa nyingi kuwalipa mawakili hatua ambayo ingesababishwa kususua kwa shughuri za ushirika.
Wamesema wanaa mini uamuzi ulioazimiwa na wanachama wa kumaliza mgogoro kwa kulipwa fidia ya eneo lililovamiwa ni msingi kwani kama suluhisho lingekosekana serikali ingeingilia kati suala hilo kwa kulirudisha kwa uma.
Wanachama wa chama cha ushirika mkoa wa Njombe
Shani Mayosa mkuu wa kitengo cha sheria vyama vya ushirika mkoani Dodoma amesema licha ya wanachama kuridhia kumuachia muwekezaji kipande chenye mzozo kwa kulipwa fidia bado tume ya maendeleo ya ushirika inatakiwa kukutana na wizara ya ardhi na halmashauri ya mji Njombe ili maamuzi yatakayotolwa yawe ya busara.
Mtandao huu umezungumza na mwenyekiti wa chama cha ushirika mkoa wa Njombe Clemence Malekela ambaye anasema ili kuepusha kuibuka mgogoro mwingine na serikali wameamua kumaliza mzozo kwa kumtaka muwekezaji kulipa fidia ya mil 222 kwani chama kina hati halali kiliyopewa na wizara ya ardhi 1961 huku muwekeza akiwa na hati 2011 aliyopewa na halmashauri ya mji wa Njombe.
contacts
email: myefuu@gmail.com
tel: 0764492051
Mtandao huu ia sahini na wewe mdau kuendelea kukupa taarifa punde zinapotokea.
0 comments:
Post a Comment