Hayo Yamesema na Mkuu wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Uhuru Ambayo Imeagizwa Kusherekea Kwa Kufanya NUsafi Ikiwa Katika Halmashauri Ya Wilaya ya Njombe Yameazimishwa katika Kituo cha Afya cha Lupembe Kwa Kufanya Usafi Katika Meaeneo Yanayozunguka Kituo Hicho.
Dumba Amesema Katika Kudhibiti Uchafuzi Wa Mazingira Kila Mtu Anatakiwa Kuwa Mlinzi Wa Mwenzie Na kuwataka Madiwani Na Wenyeviti Katika Kata na Vijiji Mbalimbali Kuunda sheria Zitakazo waongoza Kuwachukulia Hatua Watakao Kutwa Wakichafua mazingira
Kuhusu Matumizi Ya Vyoo Dumba Amesema Kuwa Kila Kaya Inatakiwa Kujenga Choo Bora Pamoja Na Kuwa na Mazoe ya Kunawa Mikono Kwani Watu wengi wameonekana wakila Uchafu Kutokana na Kutokuwa na Uataratibu wa Kunawa Mikono
Mkuu Wa Wilaya Sarah Dumba Akipanda maua
Mkurugenzi wa Halmasharui ya wilaya ya Njombe PaulMalala ,Pichani
Mbunge wa Jimbo La Lupembe Joram Hongori
Wauguzi Kituo Cha Afya Cha Lupembe
Joram Hongori Ni Mbunge Wa Jimbo Hilo Amabaye Ameongoza Zoezi Hilo Amabalo Mgeni Rasmi Alikuwa Mkuu Wa Wilaya Zoezi AmbaPO AMESEMA Limekamilika Vizuri Na Kuwataka Wananchi Hao Kalifanyia Usafi Mara Kwa mara Katika Makazi yao.
Akiongelea Juu Ya Uboreshaji Wa Kituo Hicho cha Afya Hongori Amesema Kuwa Yeye Kama Mbunge Wa Jimbo Hilo Atahakikisha anashirikiana na Halmashauri Ya Wilaya Katika Kuboresha Wodi Ya Wazazi,Jiko pamoja na Upatikanaji Wa Maji Safi Katika Kituo Hicho.
Kwa Upande wao wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho hayo ya Siku Ya Uhuru kwa Kufanya Usafi Ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli Wamesema Pongezi Za Dhati Ziende Kwa Dr Magufuli Huku Wakiitaka Serikali Kuweka Mikakati Ya Kufanya Zoezi Hilo Mara Kwa Mara Ilikukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko.
Pamoja na hayo wamesema wanamuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba Kufuatia Kuamuru Kila Mwananchi Kuwa Mlinzi wa Mwenzake katika Kudhibiti Uchafuzi wa mazingira Kwa Kumpa Asilimia 20 ya Faini Mtu atakayemkamata Mchafuzi wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment