Diwani wa kata ya Ramadhani George Sanga(wa pili kushoto na wa nne ni Dr Rajeev Singh )
Mkurugenzi mkuu wa TANWAT Dr Raveej Singh Akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kisima
Dr Rajeev Singh Akipump maji katika Kisima
Kampuni ya TANIWAT Mkoani Njombe imeukabidhi mtaa wa Kibena msaada wa kisima cha maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kupunguza uhaba wa maji katika eneo hilo.
Msaada huo umetolewa Mei 10 mwaka
huu katika eneo la mtaa huo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Dr Rajeev
Singh ambaye amesema kuwa jambo lililopelekea kutoa msaada huo kwa wananchi wa
mtaa wa Kibena ni pamoja na ushirikiano mzuri uliopo baina ya wananchi na
uongozi wa kampuni hiyo.
Dr Singh amesema endapo wananchi
hao wataendelea kudumisha ushirikiano uliopo basi uongozi wa kampuni hautasita
kuendelea kutoa misaada katika sekta mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wakazi
wa mkoa wa Njombe na taifa kwa Ujumla.
Awali akizungumza wakati wa hafla
fupi ya makabidhiano ya mradi huo diwani wa kata ya Ramadhani George sanga
amesema Kampuni hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika suala la maendeleo katika
kata yake na mkoa kwa ujumla kwani imekuwa ikitoa nafasi za ajira kwa wananchi
pamoja na kutoa misaada katika sekta mbalimbali.
Kufuatia kukamilika kwa mradi huo mheshimiwa
diwani amesema kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzie ili kuhakikisha
kisima hicho kinatunzwa huku akiwasihi wananchi kuacha tabia ya kuingiza
masuala ya kisiasa katika shughuli za kimaendeleo.
Kwa Upande wao wananchi wa mtaa huo
wameipongeza kampuni ya TANWAT kwa kuwakabidhi mradi huo kwani kabla ya hapo
walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji.
Aidha wananchi hao wameishukuru
kampuni hiyo kwa kuahidi kutoa msaada wa mbao zitakazosaidia kukamilisha ujenzi
wa ofisi ya mtaa huo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa zaidi ya asilimia 80
na kugharimu zaidi ya shilingi milion tisa za kitanzania.
@JUKUMU LETU CREW NZIMA YA MTANDAO HUU WA DARUBINI YA MTAA NIKUKUONYESHA YALE YOTE YASIONEKANA KWA URAHISI KWA KUTUMIA MACHO YAKO
0 comments:
Post a Comment