MR PUMBAFU THANA (KINYAMBE) BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI MKOANI MBEYA




Taarifa Zinasema may 12 2016 kuliibuka uvumi katika mitandao ya kijamii kwa baadhi ya waigizaji wa filamu nchini kuhusiana na kifo cha mwigizaji mahiri aliyeibuka kwa kasi ya ajbu   Mohammed Abdallah  (Kinyambe) ambaye jina lake lilianza kukua baada ya kuigiza katika "Vituko Show"

Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah  "KINYAMBE" amefariki dunia  usiku huko nyumbani kwao Mbeya.
Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitishia Saluti5 kuwa msanii huyo wa filamu ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Kinyambe alisifika kwa kuigiza filamu kama ZOBA kwa aina ya comedy zake alizokuwa akizicheza kwa kugeuza macho kama kinyonga na enzi za uhai wake alidai kuwa sababu ya yeye kuimba nyimbo za injiri ni njia pekee ya kumuimbia na kumshukuru mungu kwa kipawa alichompa.

Alishawahi kutamba katika mchezo wa vituko show na umahiri wake wa kuigiza pia ulianza kuonekana sana baada ya kushirikishwa na mwimbaji wa nyimbo za injiri kutoka mkoani mbeya katika wimbo uliopewa jina la "Acha ya Dunia" aliyoshirkishwa na mwimbaji wa kwaya ya Makongorosi Chunya Mederick Sanga.

Enzi za uhai wake alisema alibuni staili ya kuzungumza kama zuzu na kutengeneza makengeza ilikukonga nyoyo za mashabiki kwa haraka jambo ambalo anadai alifanikiwa kwa asilimia kubwa lakin kuiharisia hana ulemavu wa aina yeyote.

Kinyambe alizaliwa kutoka kwa wazazi ambao baba ni muislamu na mama mkristo. 


Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment