KOMBE LA DUNIA 2018: MCHUJO MAREKANI YA KUSINI KUENDELEA JUMANNE USIKU BILA NEYMAR!



Mechi za Kanda ya Marekani ya Kusini za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, zitaendelea tena Jumanne Usiku kwa Timu zote 10 kutinga dimbani.
Vinara Ecuador watakuwa Ugenini kucheza na Colombia wakati Timu ya Pili ipo kwao kuivaa Peru.
Brazil, ambao wako Nafasi ya 3, wako Ugenini kucheza na Paraguay ambao wako Nafasi ya 4.
Argentina, ambao wako Nafasi ya 5, wako Nyumbani kucheza na Bolivia wakati Mechi nyingine ni kati ya Venezuela na Chile.
Kwenye mfululizo wa Mechi hizi, Brazil itamkosa Nahodha wao Neymar ambae yupo Kifungoni Mechi moja baada ya kuzoa Kadi za Njano.
Kwenye Kundi hili, Timu 4 za juu zitafuzu moja kwa moja kwenda huko Urusi wakati ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo na Timu ya Bara jingine ili Mshindi aende Fainali.
MSIMAMO:
CONMEBOL-MAR28
KANDA YA MAREKANI YA KUSINI -CONMEBOL
Ratiba


Jumanne Machi 29
23:30 Colombia v Ecuador
Jumatano Machi 30 [jumanne kuamkia Jumatano]
02:00 Uruguay v Peru
02:30 Argentina v Bolivia 
02:30 Venezuela v Chile   
03:45 Paraguay v Brazil   
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment