MKUU wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewakumbusha watumishi wa
ofisi yake matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano na kuwataka wafanye
kazi kwa kuzingatia weledi na nidhamu ili kufikia mafanikio
yanayokusudiwa.
Akizungumza na watumishi hao, Masenza alisema Serikali chini ya
uongozi wa Rais John Magufuli, ina dhamira ya kweli ya kuhakikishia
watumishi wake wanatoa huduma bora kwa wananchi na si vinginevyo.
Alisema watumishi wazembe na wasiojituma, hawatapata nafasi ya
kuendelea kuwepo kazini katika uongozi huu, hivyo ni vema wakajipanga na
kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Hapa Kazi Tu ya Rais
John Magufuli.
“Hakuna mtumishi mzembe atakayesalimika kwa sababu Serikali haina
mchezo. Ni vema mkakumbuka kuwa mnatakiwa muwajibike kwa kiwango
kitakachowafanya wananchi wafurahie huduma bora, huku nchi ikisonga
mbele kwa maendeleo,” alisema.
Aliweka wazi kuwa, utawala wa sasa umedhamiria kuleta mabadiliko ya
kweli, kwa hiyo watumishi wa Serikali wanapaswa kushiriki kuleta
mabadiliko hayo na si kufanya uzembe na uvivu kwa sababu mabadiliko
yataanza nao.
Aliongeza kuwa Rais Magufuli alikwishaweka bayana kuwa hakuna
kiongozi wa juu wala mtumishi wa Serikali wa ngazi ya kati na chini
atakayefanya makosa katika uwajibikaji na kuachwa aendelee kuharibu
kazi.
Katika hatua nyingine, aliagiza ufanyike uhakiki wa watumishi katika
ofisi yake, ili kubaini endapo wapo watumishi hewa na kuelezwa sababu za
uwepo wao ilhali mifumo ya udhibiti ipo. Tumelazimika kuirudia habari
hii, kwa sababu katika gazeti letu la juzi, kichwa cha habari kilikosewa
kwa bahati mbaya. Tunawaomba radhi wasomaji wote kwa kosa hilo.
Home / Uncategories / MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA ASEMA WAFANYAKAZI WAZEMBE NA WASIOWAJIBIKA HAWAVUMILIWA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment