MWANAHISA MKUU ARSENAL, ALISHER USMANOV, ADAI WENGER NI ‘ALAMA NA MALI KUU’ YAO!
MMOJA wa Wanahisa wakubwa wa Arsenal, Alisher Usmanov, amedai Klabu hiyo bado inamhitaji Arsene Wenger.
Usmanov, mwenye Hisa Asilimia 30.05% ya Kampuni inayoimiliki Arsenal, amedai Wenger anapaswa kuhusishwa na mchakato wa kumteua Mrithi wake endapo ataamua kuondoka.
Mfanyabiashara huyo wa Urusi amesema: “Klabu lazima iibakishe alama yake kubwa na mali yake muhimu ambayo ni Arsene Wenger!”
Lakini licha ya kumsapoti Wenger, Usmanov pia amedai Arsenal inasakamwa na kushindwa kwao kwa Miaka mingi kutwaa Ubingwa wa Ligi na pia kutamka waziwazi kuwa Msimu huu nao hawatatwaa Ubingwa.
Usmanov ameeleza: “Wenger ni Kocha mzuri na Arsenal inapaswa kumpa nafasi kwenye mchakato wa Mrithi wake akiamua kuondoka.”
Akiongea kwenye Kipindi cha TV ya Rossiya24, Usmano alitamka: “Kufeli kumeisakama Arsenal kwa Miaka mingi sasa, hawawezi kuwa tena Mabingwa wa England. Hilo limeleta kutofurahishwa kwa nafasi ya Wenger kama Meneja!”
DONDOO MUHIMU:
-Klabu ya Arsenal inamilikiwa na Kampuni ya Arsenal Holdings, PLC ambayo Wanahisa wake wakubwa ni Mmarekani Stan Kroenke, mwenye Hisa 66.64% na Mrusi wa Uzbekistan Alisher Usmanov, mwenye Asilimia 30.05%
Msimu huu, tayari Arsenal wameshatupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia FA CUP, Kombe ambalo walilitwaa kwa Misimu Miwili mfululizo iliyopita.
Hivi sasa Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikizidi kuyoyoma.
Wenger, ambae amekuwa Arsenal tangu 1996, alitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya mwisho Mwaka 2004.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford
1700 Bournemouth v Man City
1700 Norwich v Newcastle
1700 Stoke v Swansea
1700 Sunderland v West Brom
1700 West Ham v Crystal Palace
1930 Liverpool v Tottenham
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton
1800 Man United v Everton
0 comments:
Post a Comment