ZAIDI YA MIL 90 PAMOJA NA VIFAA VYA UJENZI VIMEPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA UKARABATI WA SHULE YA SECONDARY WANGING'OMBE



NJOMBE      
Waziri mkuu Mstaafu awamu ya nne Mizengo Pinda ameiasa jamii ya watanzania kuwekeza katika elimu kwa watoto ili waweze kuwasaidia hapo baadae baada ya kuzeeka.
Pinda ametoa kauli hiyo akiwa katika Harambee ya kuchangia Ukarabati wa Sekondari ya Wangingombe iliyopo mkoani Njombe kutokana na hali mbaya ya uchakavu wa miundombinu yake iliyohudumu kwa zaidi ya miongo 5 na kutoa wasomi wengi wa kada mbalimbali hapa nchini.

Akiwa katika Harambee hiyo Pinda anasema kuwa taifa lolote haliwezi kufika popote kama halitaimarisha sekta ya elimu huku akiitaka serikali mkoani humo kuongeza jitihada za koboresha miundombinu ili uweze kuwa nambari moja Tanzania.
Waziri mkuu mstaafu Mizengo Piter Pinda akihamasisha wadau kuwekeza katika elimu kwa watoto wao
Kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafifi amesema tayari wameanza kufanya ukarabati wa majengo na samani nyingi chakavu lengo likiwa ni kuinua kiwango cha elimu.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri akifungua zoezi hilo la harambee katika ukumbi wa Green city makambako.
Wakizungumia hali ilivyo kwa sasa na matokeo ya baada ya kufanyika kwa ukarabati katika shule ya hiyo wadau na watumishi wengine wa serikali  wamesema kutaongeza ufaulu huku wakiwaomba wazazi na walezi kutokuwa waoga kuwekeza kwenye elimu.

Father. Evodius Msigwa – Mkiti wa kamati ya harambee akisoma taarifa ya mpango huo wa ukarabati


Katibu mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Philipo Luhanjo akifafanua juu ya hali ilivyo katika shule ya sec Wanging'ombe
Changizo hilo limekusanya zaidi ya shilingi Milioni 90 kutoka kwa wadau mbalimbali huku wengine wakichangia vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ili kukarabati shule hiyo iliyojengwa 1983 na kuwekwa jiwe la msingi 1996 na rais wa awamu ya tatu Mh Benjamin Mkapa.



Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment