MAJUKUMU MENGI YA WAZAZI IMEDAIWA KUCHANGIA ONGEZEKO LA UDUMAVU NA UTAPIAMLO MKOANI NJOMBE


           Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka Akifungua semina ya Lishe Mkoa
NJOMBE, Imeelezwa kwamba majukumu mengi ya wazazi mkoani Njombe pamoja na kutozingatia mlo kamili kumekuwa chanzo cha kuongezeka kwa watoto wenye utapiamlo na udumavu mkoani humo.

Tafiti zinaonyesha mkoa wa Njombe unashika nafasi ya pili kitakwimu katika magonjwa ya utapiamlo na udumavu huku ukiwa na 49.4% wakati mkoa kinara ukiwa ni mkoa wa Rukwa .

Neema Lazaro Mratibu  Toka Shirika la KUAM Linalotekeleza Mradi wa Tubadili Lishe Mkoani Njombe Ambaye Anasema Shughuli Nyingi za wazazi hasa akina mama  Ndizo Zinasababisha Watoto Kukosa Lishe Bora pamoja na kukosa elimu ya upangaji wa milo katika familia.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amesema utapiamlo na udumavu haukupaswa kuwepo mkoani humo kwani kila zao la chakula linapatikana hivyo wazazi na walezi wanatakiwa Kuzingatia Siku 1000 za Lishe Kwa Mtoto Tangu Mimba Inapotungwa.

Licha ya asilimia za utapiamlo kwa  mwaka jana mkoani Njombe kuonekana kushuka kutoka asilimia 52 hadi 49.4  imedaiwa Asilimia 18 za Madini Joto zimekosekana ili kukamilisha mlo kamili kwa watoto hali ambayo imetajwa Kusababisha Watoto Kupata ugonjwa huo.

                     Mratibu wa Lishe Mkoa Wa Njombe Betha NYIGU akiwasilisha report ya Mkoa
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment