NJOMBE, Imeelezwa kwamba majukumu mengi ya wazazi
mkoani Njombe pamoja na kutozingatia mlo kamili kumekuwa chanzo cha kuongezeka
kwa watoto wenye utapiamlo na udumavu mkoani humo.
Tafiti zinaonyesha mkoa wa Njombe
unashika nafasi ya pili kitakwimu katika udumavu na utapiamlo huku ukiwa na 49.4% wakati mkoa kinara ukiwa
ni mkoa wa Rukwa .
Neema Lazaro Mratibu Toka Shirika la KUAM Linalotekeleza Mradi wa
Tubadili Lishe Mkoani Njombe Ambaye Anasema Shughuli Nyingi za wazazi hasa
akina mama Ndizo Zinasababisha Watoto
Kukosa Lishe Bora pamoja na kukosa elimu ya upangaji wa milo katika familia
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole
Sendeka amesema utapiamlo na udumavu haukupaswa kuwepo mkoani humo kwani kila
zao la chakula linapatikana hivyo wazazi na walezi wanatakiwa Kuzingatia Siku
1000 za Lishe Kwa Mtoto Tangu Mimba Inapotungwa.
Licha ya asilimia za utapiamlo kwa mwaka jana mkoani Njombe kuonekana kushuka
kutoka asilimia 52 hadi 49.4 imedaiwa Asilimia
18 za Madini Joto zimekosekana ili kukamilisha mlo kamili kwa watoto hali
ambayo imetajwa Kusababisha Watoto Kupata ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment