Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure
itapatikana kama alivyoahidi.
Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu bure, Magufuli amesema,
mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo
hazijawahi kukusanywa.
Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi
huu.
Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo
zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya
barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.
Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali.
Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu
vingine vya muhimu shuleni.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment