AKINA MASAMAKI WA TRA WAPEWA DHAMANA
Mahakama kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya mapato
Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na
kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.
Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yametokana na ombi lililowasilishwa mahakamani hapo
na washtakiwa watatu wakiongozwa na aliyekuwa Kamishina wa Forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki.
Jaji wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso, amesema dhamana kwa washitakiwa hao watatu iko wazi
kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia
wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini watakaokuwa na uwezo
wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.
Watatu Hao Waliopewa Dhamana Wakiongozwa na Tiagi Masamaki ni Pamoja na aliyekuwa Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Habibu Mponezya na Bulton Mponezya Huku Wengine Ambao
Hawakuomba Dhamana Bado Wanasota Lumande.
0 comments:
Post a Comment