FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: 3 ZA SUAREZ ZAIPELEKA BARCA FAINALI!



 Image for the news result

BAO 3 za Luis Suarez Leo huko International Stadium Yokohama, Jijini Yokohama, Nchini Japan, zimeipeleka Barcelona Fainali ya Mashindo ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu, ambako watakutana na River Plate ya Argentina.
Leo Barca, wakicheza bila ya Lionel Messi na Neymar ambao wana maumivu, waliongoza 1-0 hadi Haftaimu dhidi ya Guangzhou Evergrande ya China ambayo iko chini ya Kocha wa zamani wa Brazil Luis Felipe Scolari.
Kipindi cha Pili, Suarez aliongeza Bao 2 moja likiwa la Penati.

Klabu zinazoshiriki:
-River Palate [Argentina]: Mabingwa wa Copa Libertadores
-Barcelona [Spain]: Mabingwa wa Ulaya
-Guangzhou Evergrande [China]: Mabigwa wa Asia
-TP Mazembe [Congo DR]: Mabingwa wa Afrika
-America [Mexico]: Mabingwa wa CONCACAF
-Auckland City [New Zealand]: Mabingwa wa Oceania
-Sanfrecce Hiroshima [Japan]: Wenyeji-Ni Mabingwa wa Japan
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment