Jose Mourinho amefukuzwa kama Meneja wa Chelsea Miezi 7 tangu awape Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Mreno huyo mwenye Miaka 52 alikuwa Chelsea kwa kipindi chake cha
pili baada ya kutwaa wadhifa wa Umeneja kwa mara ya Pili Juni 2013.
Msimu uliopita Chelsea ilitwaa Ubingwa ikiwa Pointi 8 mbele ya Man City lakini Msimu huu hali ni mbaya.
Wamefungwa Mechi 9 kati ya 16 za Ligi na wapo Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani.
Kipigo chao cha mwisho kilikuwa majuzi Jumatatu walipochapwa 2-1 na
Leicester City wanaoongoza Ligi wakiwa Pointi 20 mbele ya Chelsea.
Warithi wa Mourinho wanatajwa kuwa Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos.
HABARI ZA AWALI:
MOURINHO- HALI TETE: ABRAMOVICH AITISHA KIKAO CHA BODI CHA DHARURA!
Kwa mujibu wa ripoti za Magazeti ya Uingereza, Mmiliki wa Chelsea
Roman Abramovich hii Leo ameitisha Kikao cha dharura cha Bodi ya Klabu
hiyo kujadili hatima ya Meneja wao Jose Mourinho.
Meneja huyo wa Mabingwa hao wa England yupo kwenye presha kubwa baada ya Juzi kuchapwa 2-1 na Leicester City.
Kipigo hicho kimewatupa Chelsea Nafasi ya 16 kwenye Ligi wakiwa
Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani na pia wapo Pointi 20 nyuma ya
Vinara Leicester City baada ya Mechi 16 za Ligi Kuu England.
Mbali ya Abramovich, Wajumbe wengine wa Bodi ni Bruce Buck, Marina Granovskaia, Eugene Tenenbaum na Michael Emenalo.
Bodi hiyo ndio iliyoamua kwa Kura 3 kwa 2 kumrejesha tena Mourinho Klabuni Chelsea kwa mara ya pili hapo Mwaka juzi.
Ripoti hizo zimedai kuwa ikiwa Mourinho atatimuliwa hivi sasa
Chelsea itapaswa kumlipa karibu Pauni Milioni 40 kwa vile alisaini
Mkataba mpya wa Miaka Minne Mwezi Juni tu.
0 comments:
Post a Comment