Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea tena weekend ya December 12 baada ya kusimama kwa Ligi hiyo kwa zaidi ya wiki tatu, wakati Simba Sports Club wakiwa wameweka kambi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC, watani zao wa jadi Dar Es Salaam Young Africans wameweka kambi Bagamoyo ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Mgambo Shooting utakaochezwa jumamosi ya December 12 uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Yanga ambao walikuwa na wachezaji wao karibia wote kasoro Haruna Niyonzima, Donald Ngoma anayetajwa kuumia mkono mazoezi na nahodha wao Nadir Haroud hawakuwepo katika mazoezi ya December 8 uwanja wa Boko Veterani, Mtu wangu wa Nguvu naomba nikusogezee pichaz 10 za mazoezi ya Yanga ya December 8.
0 comments:
Post a Comment