Kinara mkuu wa kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria, ameonekana katika mkanda wa video uliowekwa mtandaoni.
Kwa
mara ya kwanza baada ya kimya cha mwaka mmoja hivi, Abubakar
Shekau,ameonekana akiwa amevalia magwanda ya kijeshi lakini bila ujasiri
wake wa kawaida.Shekau amekuwa mafichoni baada ya kundi lake kuvamiwa na majeshi ya muungano wa kanda ya Afrika Magharibi.
Kiongozi huyo wa Boko Haram anawashukuru wapiganaji wake ambao anasema wamekuwa ni wajasiri mno, ishara ya kukabiliwa na upinzani mkali wa majeshi ya Muungano wa Mataifa ya Magharibi.
Kundi hilo limekabiliwa vikali na majeshi ya Nigeria baada ya rais mpya wa nchi hiyo Muhamadu Buhari kutangaza vita kwa nia ya kuitokomeza kabisa jeshi hilo.
Boko Haram imesababisha vifo vya maelfu ya wakaazi wa Nigeria na mataifa wanachama wa muungano unaopambana nao mbali na kusababisha mamilioni ya watu Magharibi mwa Afrika hasa kaskazini mwa Nigeria kutoroka makwao.
Kampeini ya muungano huo umekomboa miji yote iliyokuwa imekaliwa na kundi hilo la Boko Haram.
Tangu mwaka wa 2009 kundi hilo linalaumiwa kwa vifo vya watu takriban 20,00 Pamoja Tukio La Kuwateka watoto wa kike nchini Nigeria
0 comments:
Post a Comment