Alisema pombe yenye kilevi kilichothibitishwa haiwezi kuathiri afya ya mtumiaji kama ilivyo dawa ya kulevya.
Ufafanuzi
huo ulitokana na swali la Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya maswala ya
Ukimwi,Mohammed Amour aliyetaka kujua tofauti ya kitaalamu baina ya
bangi na kiroba kutokana na jinsi zinavyowatesa watumiaji.
Mbunge
huyo wa Bumbwini Unguja alisema kuna kiwango kikubwa cha kilevi
kilichopo katika viroba kinachoweza kusababisha athari kwa watumiaji.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo kwenye ofisi ya wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, Dr. Kigwangalla alisema: "Madhara
yanatofautina, ya muda mrefu na ya muda mfupi.Utumiaji wa bangi
unaathiri mfumo wa fahamu kwenye ubongo, lakini pombe iliyopimwa kiasi
cha alkoholi haiwezi kukuathiri."
Licha
ya majibu hayo,Dr. Kigwangalla aliahidi kufuatilia suala hilo katika
mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo inahusika na vipimo
kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
"Nitafuatilia kwa kina TFDA nione wanafanyaje, kwa nini viroba vimekuwa vikiuzwa mitaani tofauti na viwango halisi vya alkoholi.Na Wanabandika asilimia sita kumbe ni asilimia hata 30 ya alkoholi.” "
Awali,
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alisema wafanyabiashara
wa viroba wamekuwa wakitumia ujanja wa kuweka nembo ya asilimia ndogo
lakini uhalisia wa kiwango cha alkoholi katika kiroba chenyewe ni
kikubwa zaidi.
0 comments:
Post a Comment