MTU mmoja amefariki kwa ugonjwa wa kimeta wilayani Rombo, huku
wengine 197 wakiwa katika uangalizi maalumu na wanne wakitambulika
kuugua baada ya kula nyama yenye vimelea vya ugonjwa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema ugonjwa huo
umeripotiwa katika vijiji vya Ubetu, Wama na Kilongo na wagonjwa
wanaendelea na matibabu katika Hospitali Teule ya Huruma.
Sadiki ambaye alifanya ziara katika wilaya hiyo, aliagiza wananchi
kutokula nyama za wanyama kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe bila
kuthibitishwa na wataalamu wa afya ili kuepusha kuenea zaidi kwa ugonjwa
huo.
Taarifa ya Sadiki iliyotumwa jana na Ofisa Habari wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Shaban Pazi, ilieleza kuwa kuna uwezekano wa kudhibiti
kuenea kwa ugonjwa huo ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na tayari chanjo kwa
mifugo inaendelea.
Alitaka wataalamu wa sekta ya afya kudhibiti uhamishwaji wa mifugo
kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hususan maeneo ya mipakani na nchi
ya Kenya ili kuhakikisha mifugo ya nchini inayopata chanjo haipati
maambukizi mengine ya ugonjwa huo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment