Bundi anaanza kukaza macho kwa Barcelona baada ya kupoteza mechi yake ya pili ndani ya mechi tatu za La Liga.
Barcelona
imekutana na kipigo cha bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Real Sociedad
ambayo ilicheza vizuri katika kipindi cha kwanza na kupata bao kupitia
Kimel Oiarzabal katika dakika ya 5.
Jitihada za Lionel Messi na Neymar kutaka kusawazisha hazikuzaa matunda hadi dakika za mwisho.
Ndani
ya mechi tatu, imepoteza mbili baada ya kuchapwa na Real Madrid kwa
mabao 2-1, ikaamka na kuitwanga Atletico Madrid 2-1 kabla ya kukutana na
kipigo cha leo.
0 comments:
Post a Comment