CHELSEA YAMPA NDOO CLAUDIO RANIERI



WALIOKUWA MABINGWA WA ENGLAND Chelsea Leo wametoka nyuma kwa Bao 2-0 na kulazimisha Sare ya 2-2 na Tottenham Hotspur ambayo ilitosha kuua matumaini ya Tottenham kutwaa Ubingwa na kuwapa Leicester City Ubingwa wao wa kwanza katika Historia yao.
Leicester, ambao chini ya Meneja kutoka Italy Claudio Ranieri aliewahi kuiongoza Chelsea, sasa wamebakisha Mechi 2 na wana Pointi 77 na hawawezi tena kukamatwa na Tottenham wenye Pointi 70 na pia kubakisha Mechi 2.
Bao la Kwanza la Spurs lilifungwa na Harry Kane kwenye Dakika ya 35 alipovunja Ofsaidi na kumzunguka Kipa Begovic na kufunga.
Dakika ya 44, Pasi ya Eriksen ilimaliziwa na Son na kuandika Bao la Pili kwa Spurs.
Hadi Mapumziko, Chelsea 0 Spurs 2.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 58, Gary Cahill aliipa Chelsea Bao kfuatia Kona na yeye kumalizia vizuri.
Chelsea walisawazisha na Gemu kuwa 2-2 kwa Bao zuri la ushirikiano ambalo Eden Hazard alifunga kwa Shuti la juu la kupinda ambalolo lilimshinda Kipa Lloris.

MAGOLI:
Chelsea 1
-Gary Cahill 58’
-Eden Hazard 83’
Spurs 2
-Harry Kane 35’
-Heung-Min Son 44’

Mechi hii iliyojaa ubabe na vitimbwi, na ambayo bila shaka Klabu na Wachezaji watalivaa rungu la FA, ilimalizika kwa Bao 2-2 na Chelsea kuhakikisha hawafungwi kwao Stamford Bridge na Spurs, Rekodi ambayo imedumu Miaka 26.
Bila shaka, kuikamata maini Spurs na kuwapa Ubingwa Leicester ndio lilikuwa lengo kuu la Chelsea na Mashabiki wao.
VIKOSI:
Chelsea: Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Mikel, Matic, Willian, Fabregas, Pedro, Costa.
Akiba: Baba, Oscar, Hazard, Traore, Kenedy, Amelia, Loftus-Cheek.
Tottenham Hotspur: Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Dier, Dembele, Lamela, Eriksen, Son, Kane.
Akiba: Mason, Vorm, N’Jie, Chadli, Wimmer, Carroll, Davies.
REFA: Mark Clattenburg
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumatatu Mei 2
Chelsea 2 Tottenham 2          
Jumamosi Mei 7
1445 Norwich v Man United                 
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Newcastle              
Bournemouth v West Brom         
Crystal Palace v Stoke                
Sunderland v Chelsea                 
West Ham v Swansea                 
1930 Leicester v Everton            
Jumapili Mei 8
1530 Tottenham v Southampton           
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Watford          
Man City v Arsenal           
Jumanne Mei 10
2145 West Ham v Man United              
Jumatano Mei 11
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Norwich v Watford  
Sunderland v Everton                
2200 Liverpool v Chelsea            
Jumapili Mei 15
**Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Aston Villa         
Chelsea v Leicester          
Everton v Norwich           
Man United v Bournemouth                  
Newcastle v Tottenham              
Southampton v Crystal Palace               
Stoke v West Ham            
Swansea v Man City         
Watford v Sunderland                
West Brom v Liverpool              
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment