BURNLEY YA KWANZA KUPANDA, YAREJEA TENA LIGI KUU ENGLAND!
BURNLEY imekuwa Timu ya kwanza kupanda Daraja na kurejea tena Ligi Kuu England ikiwa ni Siku 359 tokea waporomoshwe Daraja Msimu uliopita.
Leo Burnley waliifunga Queens Park Rangers 1-0 na kuhakikisha wao watakuwa moja ya Timu 3 zitakazopanda kutoka Daraja la Championship kwenda BPL, Ligi Kuu England.
Zikiwa zimebaki Mechi 1 kwa kila Timu, Burnley wapo kileleni wakiwa na Pointi 90 wakifuatiwa na Middlesbrough na Brighton zenye Pointi 88 kila moja na Timu hizo haziwezi kuipita Burnley kwa vile zitapambana zenyewe katika Mechi ya mwisho.
Timu 2 za kileleni za Championship hupanda Daraja moja kwa moja na Timu ya 3 hupatikana kwa Mechi maalum za mchujo zinazohusisha Timu zitakazomaliza Nafasi za 3 hadi ya 6.Bao la ushindi kwa kwa Burnley, ambayo inaongozwa na Mchezaji machachari Joey Barton aliewahi kuwa QPR, lilifungwa Dakika ya na Sam Vokes Dakika ya 61.
Mara baada ya Mechi hii iliyochezwa Nyumbani kwa Burnley, Uwanja wa Turf Moor, kumalizika Mashabiki wa Burnley walivamia Uwanja na kushangilia kwa furaha.
CHAMPIONSHIP-MSIMAMO TIMU ZA JUU:
0 comments:
Post a Comment