JAMBAZI LAUWAWA
Jeshi la polisi mkoani Njombe limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa mara wanapobaini viashiria vya uwepo wa uhalifu katika maeneo yao ili kuendelea kulinda afya za raia na mali zao.
Rai hiyo imetolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe John Charles Temu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa wananchi wanajukumu la kuripoti taarifa mapema ili kuliwezesha jeshi hilo kukabiliana na vitendo vya kiuhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu.
Kauli ya kaimu kamanda huyo imekuja kufuatia tukio la kuuawa kwa MTUHUMIWA MMOJA ANAE TAFSIRIWA KUWA NI jambazi katika tarafa ya Makambako wilaya ya Njombe mkoani hapa wakati wakikabiliana na askari waliokuwa kwenye doria ambaPO mpaka sasa MTUHUMIWA HUYO hajafahamika jina lake huku ikielezwa kuwa taarifa za kuwepo kwa uhalifu huo zilitolewa na raia wema.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda askari waliokuwa kwenye doria walipambana na majambazi watatu na kufanikiwa kumjeruhi mmoja ambaye mpaka sasa amepoteza maisha na wengine kukimbia huku wakifanikiwa silaha aina ya Long Rifle carber 22mm yenye namba za usajili A 194300 ikiwa na risasi tano ndani ya magazine hiyo.
Temu amesema kuwa kwa sasa hali ya mkoa iko salama na kwamba jeshi la polisi bado linaendelea na msako wa kuwabaini majambazi wawili waliokimbia.
0 comments:
Post a Comment