WAANDISHI WA HABARI NJOMBE WATAKIWA KUACHANA KUTANGAZA HABARI ZA PROPAGANDA NA UCHOCHEZI



Waandishi wa habari Kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoani Njombe NPC wakiendelea kunolewa na Baraza la Habari Tanzania MCT.

Na Joctan Myefu

Waandishi wa habari Mkoani Njombe Wametakiwa Kuachana na Habari za Uchochezi na Propaganda Kutokana na Kuhatarisha Usalama wa Nchi na Jamii Nzima Kwa Ujumla.

Kauli Hiyo Imetolewa na Mwezeshaji Kutoka Baraza la Habari Tanzania MCT Mzee Attilio Tagalile Muda Huu Wakati Akiendelea na Semina ya Siku Nne mjini Njombe Iliyoanza Jana Juni 16 Mwaka huu Kutokana na Wanahabari wengi kuonekana kuandika habari za uchochezi unaotokana na kununuliwa na Wanasiasa.

Bwana Tagalile Amesema Kuwa Mwandishi wa habari anatakiwa kupima kila jambo linalozungumzwa na wanasiasa majukwani kabla halijatangazwa kwenye vyombo vya habari.

Amesema katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na Amani Licha ya Vurugu zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali lakini vyombo vya habari havitakiwa kutangaza habari inayoashiria kuvuruga amani ya mahali popote na taifa kwa ujumla .

Ameongeza kuwa Vyombo vya Habari Vimekuwa Vikishindwa kutenda haki katika Kutoa taarifa za mambo mbalimbali na kujikita kumuandika mtu badala ya Mambo yanayoihusu jamii.
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment