LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumanne Mei 10
2145 West Ham v Man United
Mechi hii kwa Man United ni muhimu mno kwani wakishinda tu wataikwaa Nafasi ya 4 ya BPL, Ligi Kuu England na kufanya hatima yao ya kumaliza ndani ya 4 Bora iwe mikononi mwao kwa vile Mechi yao ya mwisho kabisa ya BPL Msimu huu ni Jumapili ijayo Uwanjani kwao Old Trafford dhidi ya Bournemouth.
Baada ya Mechi za Wikiendi ambazo West Ham walinyukwa 4-1 kwao Upton Park na Swansea City na kupoteza mwelekeo wa kupigania 4 Bora na Man City kutoka 2-2 na Arsenal na kubaki Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 2 tu mbele ya Timu ya 5 Man United yenye Mechi 1 mkononi kumufungua milango kwa Man United kuinyakua Nafasi ya 4.
-Man United hawajafungwa na West Ham katika Mechi 14 za mwisho za Ligi Uwanjani Upton Park wakishinda 11 kati ya hizo.
Mwezi uliopita, Uwanjani hapo hapo Upton Park, Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, ilitua na kuinyuka West Ham 2-1 katika Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP na United kutinga Nusu Fainali na kuichapa Everton na kusonga Fainali ambapo Mei 21 watacheza na Crystal Palace Uwanjani Wembley.
Kuelekea Mechi hii
Man United wapo kwenye wimbi zuri la kushinda Mechi 5 kati ya 6 zilizopita wakiwa wamefungwa Mechi 1 tu katika 11 zilizopita.
West Ham walikuwa hawajafungwa kwao Upton Park tangu Agosti na wakaja kufungwa na Man United kwenye FA CUP na Jumamosi kupigwa na Swansea.
Hali za Wachezaji
West Ham itamkosa Kipa wao Nambari 1 Adrian lakini anaeziba pengo lake ni Kipa Namba 1 wa Republic of Ireland, Darren Randolph.
Kwa Man United, baada ya kupumzishwa Mechi ya Jumamosi waliyoifunga Norwich City huko Carrow Road, Daley Blind na Marcus Rashford watarudi kundini huku Anthony Martial akichunguzwa baada ya kujitoa Dakika za mwisho huko Carrow Road kabla Mechi haijaanza baada kusikia maumivu wakati Kikosi kikipasha moto.
Wachezaji wa Man United watakaokosekana ni Majeruhi Matteo Darmian, Luke Shaw na Bastian Schweinsteiger wakati Marouane Fellaini akitumikia Kifungo chake cha Mechi ya Pili kati ya 3.
VIKOSI VITATOKANA NA:
WEST HAM: Randolph, Spiegel, Cresswell, Reid, Ogbonna, Collins, Tomkins, Byram, Noble, Kouyate, Obiang, Antonio, Moses, Lanzini, Payet, Sakho, Carroll, Emenike, Valencia.
MAN UNITED: De Gea, Romero, Valencia, Varela, Smalling, Blind, Jones, Rojo, Fosu-Mensah, Borthwick-Jackson, McNair, Carrick, Herrera, Schneiderlin, Lingard, Mata, Depay, Young, Rashford, Rooney, Martial.
REFA: Mike Dean
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
TIM E
Jumatano Mei 11
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Norwich v Watford
Sunderland v Everton
2200 Liverpool v Chelsea
Jumapili Mei 15
MARCH ZAKUHITISHA LIGI
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Leicester
Everton v Norwich
Man United v Bournemouth
Newcastle v Tottenham
Southampton v Crystal Palace
0 comments:
Post a Comment