KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA NJOMBE MJINI YATUPILIWA MBALI
Mei 9 Mwaka Huu ni Tarehe Iliyopangwa Kwa ajili ya Kutoa Hukumu ya Kesi Ya Uchaguzi Mkuu ya 2015 Nafasi ya Ubunge Jimbo la Njombe Mjini Baada ya Mwenendo wa Kesi Kusikilizwa Hapo Jana Kupitia Mawakili wa Pande Zote.
Mahakama Kuu Kanda Ya Iringa Mjini Njombe hapo Leo Imesikiliza Tathmini ya Mwenendo wa Kesi Namba 6 ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015 Nafasi ya Ubunge Jimbo la Njombe Mjini Ambapo Mawakili wa Pande Zote Wameeleza Majumuisho ya Mwenendo wa Kesi Hiyo.
Kesi Hiyo Iliyofunguliwa na Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Njombe Mjini Kupitia CHADEMA Emmanuel Godfrey Masonga Dhidi ya Aliyetangazwa Mshindi Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Edward Franz Mwalongo Imewaruhusu Mawakili Hao Wakiwemo Wa Serikali Kuwasilisha Mwenendo Huo Ambapo Kila Mmoja Ameonekana Kuvutia Upande Wake.
Mawakili Watatu Ndio Waliowasilisha Mwenendo wa Kesi Hiyo namna Ambavyo Ilikwenda Ambao ni Samson Retebuka Wakili wa Edward Mwalong,Edwin Swale Wakili wa Emmanuel Masonga na Wakili wa Serikali Ntuli Mwakahesya.
Mbele ya Jaji wa Mahakama Hiyo Jacob Mwambegele Mawakili Hao Wameonekana Kila Mmoja Kueleza Utetezi Wake Kupitia Ushahidi Uliotolewa na Mashahidi wa Pande Zote na Kwamba Mawakili wa Upande wa Utetezi Pamoja na Wakili wa Serikali Wakijaribu Kuishinikiza Serikali Kutupilia Mbali Kesi Hiyo Kwa Kile Walichokiita Mlalamikaji Kushindwa Kuithibitishia Mahakama Bila Kuacha Shaka Yoyote Ikiwa Wakili wa Upande wa Mlalamikaji Akiiomba Mahakama Kutengua Au Kufutilia Mbali Uchaguzi Huo Kwa Kile Alichokiita Kampeni Zilitawaliwa na Ubaguzi na Ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za
Uchaguzi
Baada ya Mawakili Hao Kueleza Kile Ambacho Kimefanyika Katika Kesi Nzima Maamuzi Yameachwa Kwa Jaji wa Mahakama Hiyo Jacob Mwambegele Ambaye Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Mei 9 Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Asubuhi Kwa ajili ya Kutoa Hukumu.
@JUKUMU LETU CREW NZIMA YA MTANDAO HUU WA DARUBINI YA MTAA NIKUKUONYESHA YALE YOTE YASIONEKANA KWA URAHISI KWA KUTUMIA MACHO YAKO
0 comments:
Post a Comment