UEFA EUROPA LIGI: LEO LIVERPOOL WATEGEMEA KAULI MBIU YAO ‘HAPA NI ANFIELD’ KUTINGA FAINALI!



Image result for jurgen klopp


MABINGWA WATETEZI SEVILLA WACHUNGULIA FAINALI!
UEFA EUROPA LIGI

Nusu Fainali
Mechi za Pili
Alhamisi Mei 5

Kuanza Saa 4 Dakika 5 Usiku [Saa za Bongo]
Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Sevilla v Shakhtar Donetsk [2-2]
Liverpool v Villarreal [0-1]

LIVERPOOL v VILLAREAL

KIKOSI cha Meneja Jurgen Klopp kinatumaini Uwanja wao wa Anfield utawapa motisha ya kupindua kipigo cha 1-0 toka Mechi ya kwanza huko Estadio El Madrigal Nchini Spain na kutinga Fainali.
Kwenye Mechi hiyo ya kwanza, Bao la Dakika za Majeruhi la Adrián López ndio limewaweka Villareal kifua mbele.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
LIVERPOOL: Mignolet; Clyne, Toure, Lovren, Moreno; Milner, Lucas, Allen; Coutinho, Firmino Sturridge.
VILLAREAL: Areola; Mario, Bailly, Ruiz, Costa; Santos, Soriano, Suarez, Trigueros; Soldado, Bakambu.
REFA: Viktor Kassai (Hungary)

SEVILLA v SHAKHTAR DONETSK
MABINGWA watetezi wa Kombe hili, Sevilla, wapo kwao Ramon Sanchez Pizjuan huko Spain wakiwania kutinga Fainali yao ya 3 mfululizo ya Mashindano haya.
Sevilla, chini ya Kocha Unai Emery, mwenye Miaka 44, wametwaa Kombe hili mara 2 mfululizo na sasa wanasaka rekodi ya kulitwaa mara 3 mfululizo.
Timu hizi zilitoka Sare 2-2 katika Mechi iliyopita na Shakhtar, chini ya Kocha Mircea Lucescu, mwenye Miaka 70, ambae yupo kwenye hatamu tangu 2004, ni timu kigaga iliyotwaa Ubingwa wa Ukraine mara 8, Kombe la Nchi mara 5 pamoja na UEFA CUP Mwaka 2009.
Hata hivyo, Sevilla, wapo kwao na wana faida kubwa ya Bao 2 za Ugenini na hivyo Sare za 0-0 au 1-1 zitawafikisha Fainali.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
SEVILLA: Soria; Mariano, Rami, Carrico, Escudero; Krychowiak, N’Zonzi; Vitolo, Banega, Konoplyanka; Gameiro
SHAKHTAR DONETSK: Pyatov; Srna, Kucher, Rakitskiy, Ismaily; Malyshev, Stepanenko; Marlos, Kovalenko, Taison; Ferreyra
REFA: Björn Kuipers (Netherlands)

KALENDA
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment