UEFA CHAMPIONZ LIGI: FAINALI NI EL DERBI MADRILEÑO, REAL V ATLETICO, CITY YATUPWA NJE!



 Gareth Bale celebrates Real Madrid’s winner.
 WENYEJI Real Madrid wakiwa kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain, wameshinda Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL,1-0 dhidi ya Manchester City na kutinga Fainali ambayo itakuwa ni ‘El Derbi Madrileño’, Dabi ya Madrid, kwani watapambana na Mahasimu wao Atletico Madrid.
Mahasimu hao walikutana kwenye Fainali nyingine Msimu wa 2013/14 na Real kuibuka kidedea kwa Bao 4-1 baada ya Dakika za Nyongeza 30 kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 90 za Gemu.
Juzi, Atletico walifungwa 2-1 na Bayern Munich huko Munich kwenye Nusu Fainali nyingine ya UCL lakini wamesonga Fainali kwa Bao la Ugenini kwa vile walishinda 1-0 katika Mechi ya kwanza na hivyo, Gemu 2 kuwa na Jumla ya Bao 2-2, na Bao lao la Ugenini kuwapenyeza.
Hapo Jana, ndani ya Santiago Bernabeu iliyocheua Mashabiki wengi wakiwa ‘wehu’ wa Real, City walipata pigo la mapema walipolazimika kumbadili Kepteni wao Vincent Kompany alieumia na kuingizwa Eliaquim Mangala katika Dakika ya 11.
Dakika ya 20 pasi ya Carvajal ilimkuta Gareth Bale ambae alipiga vizuri Mpira wa juu ambao ulimparaza Fernando na kumshinda Kipa Joe Hart na kugonga Posti na kuipa Bao Real Madrid.
Hadi Haftaimu, Real 1 City 0.
Kipindi cha Pili Real walikosa Bao kadhaa kupitia Bale, aliepiga Posti, na nyingine Kipa wa City Joe Hart kuokoa michomo ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo alieanza Mechi hii baada ya kuzikosa Mechi 3 zilizopita kutokana na maumivu ya Musuli.
Fainali ya UCL itachezwa huko San Siro Mjini Milan Nchini Italy Jumamosi Mei 28.
VIKOSI:
Real Madrid: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric [Kovacic, 88’], Kroos, Isco [Rodriguez, 67’], Bale, Ronaldo, Jese [Vazquez, 56’].
Akiba: Casilla, Varane, James Rodriguez, Kovacic, Lucas Vazquez, Danilo, Borja Mayoral.
Manchester City: Hart, Sagna, Kompany [Mangala, 11’], Otamendi, Clichy, Fernando, Fernandinho, Toure [Sterling, 61’], Navas [Iheanacho, 69’], De Bruyne, Aguero.
Akiba: Caballero, Mangala, Kolarov, Delph, Sterling, Bony, Iheanacho.
REFA: Davir Skomina [Slovenia]
Fainali
Jumamosi Mei 28

Saa 3 Dakika 45 Usiku
Atletico Madrid v Real Madrid
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment