CAF CC: SARE YA MEDEAMA NA MO BEJAIA YAIDIDIMIZA YANGA MKIANI!

Timu za Medeama ya Ghana na MO Bejaia Leo zimetoka Sare 0-0 huko TNA Park Mjini Tarkwa Nchini Ghana katika Mechi ya Kundi A la Mashindano ya Klabu Barani Afrika ya KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC.
Timu hizi ziko Kundi pamoja na Yanga na TP Mazembe ambazo zilikutana Jana Jijini Dar es Salaam na TP Mazembe kushinda 1-0.
Baada ya Mechi 2 kwa kila Timu, TP Mazembe wanaongoza Kundi A wakiwa na Pointi 6, MO Bejaia Pointi 4, Medeama 1 na Yanga 0.
Katika Mechi zao, Yanga walianza kufungwa huko Algeria 1-0 na MO Bejaia na Jana Bao lililoiua Yanga walipocheza na TP Mazembe lilifungwa Dakika ya 75 na Merveille Bope.   
Mechi zinazofuata ni Julai 15 wakati Yanga wakiikaribisha Medeama Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Julai 17 ni huko Algeria kati ya MO Bejaia na Medeama.

Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment