TOKA TFF: MALINZI KUONGEA NA WANAHABARI, 23 WA TWIGA STARS KWENDA KIGALI WATAJWA

PRESS RELEASE NO. 133                                                                                         JUNI 29, 2016

MALINZI NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho Juni 30, 2016 saa 5.00 asubuhi atazungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF. Waandishi wa vyombo vyote mnakaribishwa.
KIKOSI CHA TWIGA STARS
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.
Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.
Makipa:
Fatma Omary
Belina Julius
Najiat Abbas
Walinzi:
Stumai Abdallah
Fatma Issa
Anastazia Antony
Happuness Henziron
Maimuna Khamis
Viungo:
Donisia Daniel
Amina Ali
Amina Ramadhani
Fatuma Bashiri
Wema Richard
Fadhila Hamadi
Mwajuma Abdallah
Anna Hebron
Sophia Mwasikili
Washambuaji:
Tumaini Michael
Johari Shaaban
Fatma Idd
Shelder Bonifdace Mafuru
Asha Saada Rashid
Mwanakhamisi Omar

Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment