Mwenge wa uhuru hii leo umehitisha ziara yake kwa kupitia miradi katika halmashauri ya wilaya wanging'ombe ukitokea wilayani makete ambapo makabidiano yamefanyika katika kijiji cha mafinga wilayani humo
Mapema hapo kesho mwenge utakabidhiwa tena katika halmashauri za wilaya ya njombe na makambako ambapo utahitisha ziara katika mkoa wa njombe na kukabidhiwa katika mkoa wa Iringa baada ya kufanikisha mapitio ya miradi yenye thamani ya bilioni saba na milioni miatano kwa mkoa mzima
Katika kijiji cha igagala kata ya ulembwe mwenge umezindua kituo cha afya cha thamani ya shilingi milioni mia mbili arobaini
Wakizungumza na kituo hiki muda mfupi baada ya jiwe la msingi kuwekwa na kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wamesema kuwa wataendelea kuchangishana mpaka ukarabati ukamilike zaidi wananeleza mchungaji Festo mpinga na Valentina mlelwa
Taarifa iliyosomwa mbele ya mwenge wa uhuru imeeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 83 zimechangwa na wananchi wa kata hiyo na ungali unahitaji kupigwa jeki
kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge george jacksoni mbijima amewataka wakazi wa kata ya ulembwe kuendelea kuchangia shuguli za maendeleo huku akiagiza halmashauri kuwaongezea fedha wananchi katika mradi
kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge george jacksoni mbijima amewataka wakazi wa kata ya ulembwe kuendelea kuchangia shuguli za maendeleo huku akiagiza halmashauri kuwaongezea fedha wananchi katika mradi
mwenge wa uhuru mwaka 2016 katika halamshauri ya wangingombe umepitia katika miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 .1
0 comments:
Post a Comment