WENYEJI France wa Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, Leo wamewamwaga Mabingwa wa Dunia Germany katika Nusu Fainali ya pili iliyochezwa huko Stade Velodrome Mjini Marseille na kutinga Fainali kucheza na Portugal
Licha ya Germany kutawala Kipindi cha Kwanza, France walipata Bao lao kwa Penati pale Refa wa Italy Nicola Rizzoli alipoamua Bastian Schweinsteiger ameunawa Mpira wa Kona akijaribu kuokoa Kichwa cha Patrice Evra.
Penati hiyo ilipigwa na kufungwa na Antoine Griezmann katika Dakika ya 47 ya Kipindi cha Kwanza.
Hadi Mapumziko Wenyeji France 1 Mabingwa wa Dunia Germany 0.
Germany waliendelea kutawala lakini wakapigwa Bao la Pili Dakika ya 72 kufuatia ufundi mkubwa wa Paul Pogba na Antoine Griezmann kuudonyoa na kutinga wavuni.
France watacheza Fainali na Portugal ambayo Jumatano iliifunga Wales 2-0 katika Nusu Fainali ya Kwanza.
VIKOSI:
GERMANY: Neuer, Kimmich, Boateng, Howedes, Hector; Kroos, Can, Schweinsteiger; Muller, Ozil, Draxler
Akiba: Leno, Mustafi, Khedira, Schurrle, Podolski, Weigl, Tah, Gotze, Sane, Gomez, Ter Stegen
FRANCE: Lloris, Sagna, Koscielny, Umtiti, Evra; Pogba, Matuidi; Sissoko, Griezmann, Payet; Giroud
Akiba: Mandanda, Jallet, Rami, Kante, Cabaye, Gignac, Martial, Schneiderlin, Mangala, Digne, Coman, Costil
Refa: Nicola Rizzoli (Italy)
EURO 2016
NUSU FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo
Jumatano Julai 6
(Stade de Lyon)
Portugal 2 Wales 0
Alhamisi Julai 7
(Stade Velodrome, Marseille)
Germany 0 France 2
FAINALI
Jumapili Julai 10
**Saa 4 Usiku, Saa za Bongo
(Stade de France, Paris)
Portugal v France
0 comments:
Post a Comment