Ni wazi kwamba mshirika na msiri wa Siku nyingi wa Jose Mourinho Rui Faria ndie atakuwa Meneja Msaidizi wa Manchester United chini ya Meneja huyo mpya huko Old Trafford.
Cheo hicho kilikuwa kikishikiliwa na Ryan Giggs aliekishika chini ya Mameneja waliotimuliwa David Moyes na Louis van Gaal.
Faria amekuwa pamoja na Jose Mourinho tangu huko Barcelona Mwaka 1996 wakienda pamoja kila Klabu aliyoenda Mourinho tangu wakati huo.
Wengine kwenye Benchi la Ufundi la Man United chini ya Jose Mourinho ni Silvino Louro ambae alianza kama Kocha wa Makipa, Ricardo Formosinho, Carlos Lalin, Emilio Alvarez na mchunguzi Giovanni Cerra.
Timu hiyo ya Mourinho ndio imepewa jukumu la kuifufua Man United na kuifanya iwemo kwenye mbio za Ligi Kuu England kitu ambacho wamekikosa tangu astaafu Sir Alex Ferguson Mwaka 2013.
Msimu uliopita Man United ilimaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kukosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wa 2016/17 na sasa watacheza UEFA EUROPA LIGI kuanzia Hatua ya Makundi.
MAN UNITED - TAREHE MUHIMU:
16 JULAI: Wigan v Man United
22 JULAI: Man United v Borussia Dortmund huko Shanghai Stadium, China
25 JULAI: [Ugenini] Man United v Man City huko Beijing National Stadium, China
3 AGOSTI: Mechi ya Kumuenzi Wayne Rooney v Everton Uwanjani Old Trafford
7 AGOSTI: Ngao ya Jamii v Leicester Wembley Stadium
13 AGOSTI: Mechi ya Ufunguzi Ligi Kuu Ugenini na Bournemouth
20 AGOSTI: Mechi ya Kwanza ya Ligi Old Trafford na Southampton
26 AGOSTI: Droo ya Makundi UEFA EUROPA LIGI
31 AGOSTI: Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho
10 SEPTEMBA: Dabi ya Manchester v Man City Old Trafford.
15 SEPTEMBA: Mechi za Makundi EUROPA LIGI zinaanza
21 SEPTEMBA: Kombe la Ligi Raundi ya 3
15 OKTOBA: Mechi Anfield na Liverpool
22 OKTOBA: Mourinho Stamford Bridge kwa mara ya kwanza kuivaa Chelsea.
26 DESEMBA: Mechi ya Boksingi Dei na Sunderland Old Trafford.
2 JANUARI: Mechi ya kwanza Olympic Stadium na West Ham.
7 JANUARI: FA Cup Raundi ya 3 Man United kuanza kutetea Taji
14 JANUARI: United v Liverpool Old Trafford
25 FEBRUARI: Dabi ya Manchester Etihad Stadium
26 FEBRUARI: Fainali ya Kombe la Ligi Wembley
21 MEI: Mechi ya mwisho ya Ligi Ugenini na Crystal Palace.
24 MEI: Fainali ya EUROPA LIGI huko Friends Arena, SJumatanoen, Sweden
27 MEI: Fainali ya FA CUP Wembley
0 comments:
Post a Comment