ISHU YA MBWANA SAMATA KUTUA AS ROMA IKO HAPA






Wakati suala la mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa njiani kutua AS Roma ya Italia likiendelea kusambaa mitandaoni, meneja wake amesema ni uzushi mtupu.

Jamal Kisongo ambaye ni meneja na mlezi wa Samatta, amesema hakuna lolote kuhusiana na hilo na Samatta anaendelea na maandalizi katika kikosi chake cha KRC Genk kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

“Nimesikia pia, kuna watu kadhaa wameniuliza pia. Lakini ukweli ni hivi; Mbwana anaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Ubelgiji.

“Hakuna lolote kuhusiana na Roma hadi sasa labda kama litakuja baadaye. Mawakala wake wote wanalijua hilo.

“Timu haiwezi ikafanya mawasiliano ya kumuuza bila ya kuwaeleza mawakala wake, meneja wake. Ndiyo maana nasema labda suala hilo lije baadaye,” alisema Kisongo.



Kuanzia leo asubuhi, taarifa za AS Roma ya Italia imekuwa kwenye mazungumzo Genk namna ya kumnasa Samatta ambaye ni nahodha wa taifa Stars, zimekuwa zikisambaa kwa kasi.
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment