Kuhusu sakata la Jerry Muro kuna taarifa zimeibuka kuwa Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia Mwaka Mmoja na kumtwanga Faini ya Milioni 3 Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro.
Kikao cha Kamati hiyo ya TFF kilifanyika Leo chini ya Wakili Wilson Ogunde Jijini Dar es Salaam bila Muro kuhudhuria kwa vile alikuwa na udhuru mwingine.
Muro anadaiwa kudharau Maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF Mwaka 2015 alipoamriwa kulipa Faini ya Shilingi Milioni 5 alipokutwa na Hatia na kutolipa Fedha hizo kitu ambacho Taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga alibainisha kuwa ilishalipwa.
Mengine yaliyomsulubu Muro ni yale yaliyohusu kuelekea kwa Mechi ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho ambayo Yanga waliamua Mechi hiyo iwe bure kwa Mashabiki wote.
Kwenye Taarifa ya Manji, kuhusu Jerry Muro, ilisomeka:
2. KUITWA KWA JERRY MURRO KATIKA KAMATI YA MAADILI YA TFF AKIWA MKURUGENZI WA HABARI WA KLABU
2.1. Hati za TFF za kuitwa kwa Jerry Murro hazionyesha wazi sababu ya Mkurugenzi wa Habari huyo wa Yanga kutakiwa kufanya hivyo ambapo atakuwa akihudhuria si kwa cheo chake katika klabu, lakini ifahamike wazi kwamba Yanga haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe kushiriki katika shughuli za soka. Tukiwa kama klabu tuko tayari hata kuunga mkono hatua zozote za kisheria dhidi ya TFF na iwapo TFF itajaribu kuifungia Yanga, tutalichukua suala hili hadi katika vyombo vya juu zaidi vya michezo.
2.2. Hata hivyo, iwapo kuitwa huko kunahusu suala la faini ya Sh. 5 Milioni dhidi ya Jerry, fedha hiyo ilikwishatolewa kwa TFF.
2.3. Wanaokula njama ndani ya TFF kuwanyamazisha au kuwafungia ambao wanaeleza mawazo yao kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, lazima wafahamu kwamba kuikosoa TFF hakupingani na sheria, na wafahamu pia kwamba Yanga chini ya uenyekiti wangu haitakubali wanachama au wafanyakazi wa klabu kudhalilishwa au kutishwa.
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment