KAMPUNI
ya Azam TV jana imeingia mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya
Sh. Milioni 23 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuendelea kurusha
moja kwa moja Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao ndani yake kuna
ongezeko la dau kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo.
Mkurugenzi
wa Azam Media, Tido Mhando alimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestine
Mwesigwa mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 23 na kusema kwamba msimu mpya
utakuwa na mabadiliko makubwa kwenye urushaji wa matangazo ya Ligi Kuu.
Mhando
alisema katika Mkataba wa awali, kila klabu ilikuwa inapata Sh Milioni
100 kwa msimu, lakini sasa kila klabu itaingiza karibu mara mbili ya
fedha hizo.
“Katika
mkataba uliosainiwa leo, klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu
ambayo ni Sh milioni 126. Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa
mfumo tofauti ambao utakuwa hivi. Timu inayoshika nafasi ya juu katika
msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi
chini,”alisema Mhando.
Alisema
ligi itakapokwisha, timu zitazokuwa juu katika msimamo zitapata fedha
nyingi kuliko za chini, ambazo zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu na
kwamba lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi
kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi, hali itakayochangia
ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili
mwisho wa ligi ifaidike.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa akipokea mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 23 kutoka kwa Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando (kushoto) |
0 comments:
Post a Comment