VPL: MABINGWA YANGA, VINARA SIMBA USHINDI, STAND ‘WAILA’ AZAM!

Image result for simba vs mbeya city 

VPL: LIGI KUU VODACOM Matokeo:
Jumatano Oktoba 12

Mbeya City 0 Simba 2
Mwadui FC 2 African Lyon 0
Mbao FC 3 Toto Africans 1
Maji Maji FC 0 Kagera Sugar 1
Stand United 1 Azam FC 0
JKT Ruvu 0 Tanzania Prisons 0
Yanga 3 Mtibwa Sugar 1

VINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba Leo wameendelea kujichimbia kileleni baada ya kuifunga Mbeya City wakati Mabingwa Watetezi Yanga wakijikusanya kwa ushindi toka kwa Mtibwa Sugar huku Azam FC wakizidi kudidimia baada ya kufungwa na Stand United iliyojizatiti kushangaza na kuwania Ubingwa.
 
Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Uhuru, Yanga, waliitwanga Mtibwa Sugar Bao 3-1 walipoongoza 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Mzambia Obrey Chirwa akifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi ambalo alipachika Dakika 1 kabla Haftaimu. 

Kipindi cha Pili Mtibwa Sugar walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Harun Chanongo lakini Simon Msuva akaipa Yanga Bao la Pili Dakika ya 68 na Mzimbabwe Donald Ngoma, aliengizwa kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa aliipa Yanga Bao la 3.

Huko Sokoine, Mbeya, Bao za Kipindi cha Kwanza za Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya ziliipa Simba ushindi wa 2-0.

Nao Azam FC, Timu inayofifia vibaya Msimu huu, ilitunguliwa 1-0 na Stand United, Timu inayokuja juu mno na imo kwenye mbio za Ubingwa, kwenye Mechi iliyochezwa huko Kambarage, Shinyanga.

Matokeo haya yamewachimbia Simba kileleni wakiwa na Pointi 20 kwa Mechi 8, wakifuata Stand United wenye Pointi 19 kwa Mechi 9, kisha Kagera Sugar wana Pointi 15 kwa Mechi 9 na Yanga wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 14 kwa Mechi 7.

Mtibwa Sugar ni wa 5 wakiwa na Pointi14 kwa Mechi 9.


VPL
YANGA - Mechi zao:
Okt 16 Yanga v Azam FC
Okt 19 Toto African v Yanga
Okt 22 Kagera Sugar v Yanga
Okt 26 Yanga v JKT Ruvu
Okt 29 Yanga v Mbao FC
SIMBA - Mechi zao:
Okt 15 Simba v Kagera Sugar
Okt 20 Simba v Mbao FC
Okt 23 Simba v Toto African
Okt 29 Mwadui v Simba
Nov 2 Stand United v Simba

VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Alhamisi Oktoba 13
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment