CITY-CHELSEA RABSHA: CHELSEA ‘YAPANCHI’ KUFYEKWA POINTI, WAPIGWA FAINI!


CITY-CHE-VITAChelsea wametozwa Faini ya Pauni 100,000 na Manchester City kutakiwa pia kulipa Faini ya Pauni 35,000 kutokana na vurugu zilizotokea kati ya Timu yao na Manchester City kwenye Mechi ya Ligi ambayo wao waliifunga City 3-1 huko Etihad Wiki iliyopita.
Kabla ya Hukumu hii, ilihofiwa mno kuwa Chelsea wanaweza kukatwa Pointi kwa vile kwa Chelsea Mashitaka ya aina hiyo yalikuwa ni ya 5 kwao ndani ya Miezi 19 iliyopita.
Lakini safari hii, inaelekea Jopo Huru la FA, Chama cha Soka England, kimeichukulia Chelsea kama si ‘mchokozi’.
HABARI ZA UNDANI BAADAE
/////////////////////////////////////////
CHELSEA HATARINI KUFYEKWA POINTI NA FA!
VINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, wapo hatarini kukatwa Pointi kutokana na vurugu zilizotokea kati ya Timu yao na Manchester City kwenye Mechi ya Ligi ambayo wao waliifunga City 3-1 huko Etihad Wiki iliyopita.
Ikiwa hilo litatimizwa na FA, Chama cha Soka England, Chelsea watakuwa Timu ya kwanza kupata Adhabu ya kukatwa Pointi za Ligi tangu Mwaka 1990.
Wiki iliyopita Chelsea na Man City zilifunguliwa Mashitaka ya kushindwa kudhibiti Wachezaji wao kwenye Mechi hiyo na kwa Chelsea Mashitaka ya aina hiyo ni ya 5 kwao ndani ya Miezi 19 iliyopita.
Vurugu kwenye Mechi hiyo ziliibuka mara baada ya Fowadi wa City Sergio Aguero kumchezea Rafu Beki wa Chelsea David Luis.
Imedaiwa vurugu hizo zilihusisha Wachezaji wote 22 wa pande zote mbili, Marizevu kadhaa na hata Maafisa wa Timu hizo waliokuwa wameketi Mabenchi ya Ufundi.
Baada ya rabsha hizo, Aguero na Mchezaji mwenzake wa City Fernandinho walitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hii sasa ni mara ya 5 kwa Chelsea kusulubiwa kwa Kosa la Kushindwa Kudhibiti Wachezaji wake ambalo ni kinyume na Sheria ya FA Kifungu E20.
Mara zote 4 walizoshitakiwa, Chelsea walipatikana na hatia na kutwangwa Faini.
Safari hii Chelsea wapo hatarini kupewa Adhabu kali zaidi ikiwemo kukatwa Pointi kama walivyofanywa Arsenal na Manchester United Miaka 26 iliyopita kwa makosa kama haya ya Chelsea.
Mara ya mwisho kwa Chelsea kuadhibiwa kwa Kosa kama hili ni baada ya vurugu za Dabi ya London dhidi ya Tottenham Msimu uliopita.
Wakati huo, Chelsea walikata Rufaa kupinga Adhabu yao ya Faini ya Pauni 375,000 na ikapunguzwa hadi 290,000 wakati Spurs walilipa 175,000 lakini Chelsea walipewa onyo kali kuhusu Rekodi yao mbovu ya kushindwa Kudhibiti Wachezaji wao na kuonywa kwamba wanaweza kukatwa Pointi makosa hayo yakijirudia.
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment