LICHA YA RAIS KUTOA AGIZO MACHINGA KUTOBUGUDHIWA LAKIN SHERIA WANATAKIWA KUZIZINGATIA

Ikiwa siku mbili zimepita tangu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli atoe agizo  kwa serikali kutowabugudhi wajasiliamali wadogo maarufu kwa jina na Machinga ,Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Edward Frana Mwalongo amewataka wafanyabiashara hao kufuata sheria ili waweze kufanya biashara zao kwa uhuru.

Image result for EDWARD FRANZ MWALONGOImage result for EDWARD FRANZ MWALONGO

Mwalongo ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara katika mtaa Posta kati ambapo  amesema kauli ya rais haitoi ruhusa kwa wafanyabiashara hao kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa na halmashauri husika hivyo ili waweze kufanya biashara bila ya usumbufu wanataiwa kuridhiana na serikali .

Pamoja na mambo mengine Mbunge huyo amewataka wananchi hao kufanya kazi kwa nguvu zao zote kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuendana na kauli mbiu ya Mheshimiwa raisi ya hapa kazi tu.

Awali akisoma taarifa ya mtaa kwa mgeni rasmi mtendaji wa Mtaa huo Elias Chilatu amesema licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki mtaa umefanikiwa kufanya shughuri nyingi za maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi ya mtaa .

Kwa upande wao wananchi wamesema wamefurahishwa na ujio wa mbunge katika mtaa wao kuwashukuru kwa kumchagua na kusikiliza kero zao na kudai wangependa mbunge huyo kuanza kuzitafutia majawabu kero za Miundombinu ya barabara na usafi.

Katika ziara hiyo Mwalongo ameahidi kutoa mifuko hamsini ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya mtaa ambayo inahitaji zaidi ya mil tisa ili iweze kukamilika.   

Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment