Polisi kutoka kituo cha Kati, Dar es salaam wakiambatana na Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Ndugu Maxence Melo, walifika katika ofisi za Jamii Media kwa ajili ya ukaguzi Jumatano.
Kwa mujibu wa mtandao, zoezi hilo limefanyika sambamba na kuwahoji wafanyakazi (Social Media Engagers na Content Quality Controllers) juu ya utendaji wa shughuli zao za kila siku.
Baada ya ukaguzi na mahojiano, polisi wameondoka na nyaraka za usajili wa Jamii Media ikiwemo cheti cha mlipa kodi, cheti cha BRELA, leseni ya biashara, n.k.
Polisi walielekea nyumbani kwa Maxence Melo ambapo napo walifanya ukaguzi ndani ya nyumba. Katika zoezi zima la ukaguzi, sehemu zote mbili, Jeshi la polisi halikuhitaji wala kuchukua kifaa cha mawasiliano ya kimtandao kama router, flash, hard disc, au kompyuta.
Msafara huo ulielekea polisi kituo cha kati kukamilisha mahojiano kati ya Mkurugenzi na wafanyakazi wawili waliochukuliwa.
0 comments:
Post a Comment