KEPTENI wa zamani wa England John Terry amemtetea Wayne Rooney na kutaka Watu wampe heshima zaidi.
Terry, ambae pia ni Kepteni wa Chelsea, ametoa Msimamo huu
baada ya Jumamosi iliyopita baadhi ya Mashabiki kumzomea Rooney wakati
England inaifunga Malta 2-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la Nchi za Ulaya
zinazowania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
iliyochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.
Leo England ipo kwenye Mechi nyingine ya Kundi lao ya Mechi
hizi za kufuzu Kombe la Dunia itakayochezwa Ugenini na Slovenia, na
Kocha wa England, Gareth Southgate, ametoboa Rooney atakuwa Benchi.
JE WAJUA?
-Rooney ndie Mfungaji Bora katika Historia ya England akiwa na Bao 53 akifuatiwa na Sir Bobby Charlton aliefunga Bao 49.
-Pia ndie Mchezaji wa Pili kuichezea Mechi nyingi England akiwa amecheza Mechi 117 na kuwa nyuma ya Kipa Peter Shilton aliecheza Mechi 125.
Akiandika
kwenye Mtandao wa Instagram, Terry, ambae alistaafu kuichezea England
Mwaka 2012, ameeleza: “Wayne Rooney, ndie Mfungaji Bora England katika
Historia ya Gemu yetu. Karibuni atakuwa ndie Mchezaji aliechezea Mechi
nyingi Nchi yetu tukufu."
"Ni mmoja wa Wachezaji Bora kabisa niliopata kuwaona maishani mwangu na ni Mtu aliejitolea kila kitu kwa ajili ya England."
"Ni Lejendari huko Everton, Man Utd, England na Soka la
Dunia. Wote tumwoshe heshima kubwa zaidi kwa Mchezaji na Mtu huyu Bora.
Kesho tuwe nyuma ya Wayne na England!"
Jana, wakiongea huko Ljubljana, Slovenia Southgate
alisisitiza kuwa Rooney bado anahitajika na England wakati Rooney
mwenyewe akisisitiza bado hajaisha.
Rooney alinena: "Nimechezea England Miaka 13 mfululizo bila
kupumzika na kujitolea kila kitu. Unafika wakati unakuwa si Jina la
kwanza kwenye Timu kama nlivyokuwa huko nyuma. Nimefanya hivyo mara 117
lakini mambo hubadilika na kilichobaki ni kufanya juhudi zaidi."
“Sifedheheki na hili. Naskia fahari kubwa kuichezea Nchi
yangu. Kama ikiwa toka Benchi itakuwa toka Benchi. Hakuna
kilichobadilika kuhusu hatima yangu. Hii ni sehemu ya Soka."
"Nina Miaka 30 na si 35 au 36 ambayo unawaza Je nitarejea? Nitaendelea kuichezea England!"
0 comments:
Post a Comment