AKINA MAMA WILAYANI LUDEWA WAHIMIZWA KUJIFUNGULIA HOSPITALINI


NJOMBE,Ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na akina mama kujifungulia majumbani kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa      Amour Hemed Hemed amewataka watu wote wenye utamaduni huo kuachana nao ili kunusuru vifo vitokanavyo na uzazi. 

Kiongozi huyo ametoa rai huyo Wilayani Ludewa kwa wakazi wa kijiji cha Madope mara baada ya kuzindua jengo la hospitali ya mama na mtoto lililogharimu zaidi ya shilingi Milioni 37 na kuwataka wanawake wa kijiji hicho wenye utamaduni huo kuelimishana juu ya madhara ya kitendo hicho.

Nao Wakazi wa kijiji cha Madope Wilayani Ludewa Mkoani Njombe ambao wamefanikiwa kujenga zahanati kwa ajili ya kurahisisha huduma za afya kwa kina mama na watoto wamesema wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 20 kupata huduma za afya hali ambayo iliwawia vigumu wajawazito.


Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake Mkoani Njombe na kukabidhiwa Mkoani Ruvuma ambapo ukiwa mkoani Njombe umekagua, umezindua na kutembelea miradi 55 yenye thamani ya zaidi ya shilingi ya BILIONI 8 na milioni 674. 


Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment