MADIWANI WASUSIA UJUMBE WA MKUU WA WILAYA KATIKA KIKAO CHA BARAZA



NJOMBE, Katika Hali Isiyo ya Kawaida Madiwani wa Chama Kikuu Cha Upinzani Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Wamesusia Kikao Cha Baraza la Madiwani Kwa Dakika Kadhaa Wakati Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri Akitoa Salaam za Serikali Kwa Kile Walichosema Walishatangaza Kutofanya Kazi na Mkuu Huyo.

Miezi Kadhaa Iliyopita Chama Cha CHADEMA Wilaya ya Njombe Kilitangaza Kutofanyakazi na Mkuu Huyo wa Wilaya Kuanzia Ngazi ya Wajumbe,Wenyeviti na Madiwani Kutoka Katika Chama Hicho Wakidai Kuwa Alimpiga Mwenyekiti Wao wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni  baada ya kubaini anaendelea na kazi huku akiwa amefungwa kifungo cha nje hali iliyopelekea kumpa siku saba mkuu huyo wa wilaya kukiomba radhi chama hicho na kushindwa kufanya hivyo.

Mara baada ya Mkuu wa Wilaya kumaliza kutoa salamu za serikali kuu madiwani hao wakarejea katika kikao na kuibuka tena mabishano ya zaidi ya Saa moja wakipinga mkuu huyo kuchangia kila hoja inayojadiliwa katika kikao wakidai ni kinyume cha sheria bila ya kukubaliwa na baraza la Madiwani Katika halmashauri Hiyo Jambo Lililomlazimu Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Bwana Edwin Mwanzinga Kukubaliana na Malalamiko ya Upinzani Kwa Kumtaka Mkuu wa Wilaya Kutochangia Hoja Yoyote.

                             Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri wa Kwanza kushto 
Akifafanua kifungu cha sheria kinachomhusu mgeni muarikwa Mwanasheria wa halmashauri hiyo
moris milanzi amesema katika kifungu cha sheria 27(1) cha kanuni za kudumu za halmashauri kinampa ruhusa mwenyekiti kumruhusu mgeni kuhudhuria na kuchangia jambo lolote isipokuwa hataruhusiwa kupiga kura.

Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment