Na Joktan Muyefu,
NJOMBE, Zikiwa ni jitahada za kufanya mji kuwa safi muda wote halmashauri ya mji mdogo wa Makambako imesema ipo katika hatua za mwisho za kununua trekta kwa ajili ya kuzoela taka katika maeneo mbalimbali ya mji huo wa kibiashara uliyopo mkoani Njombe.
Chesko Hanana Mfikwa ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako amesema kukithiri kwa taka katika mji huo kumetokana na shughuri za kibiashara zinazoendelea hali ambayo imekuwa tishia kiafya na kuwalazimu kutuma maombi TAMISEMI ya kuruhusiwa kununua trekta litakalosaidia operesheni ya usafi mjini hapo.
Sambamba na hilo mwenyekiti huyo amemtaka mkurugenzi kutobadili matumizi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya kuzolea taka kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa yatokanayo na mlundikano wa takataka katika vizimba.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Njombe CHESKO HANANA MFIKWA
Nao wananchi wamesema mlundikano wa takataka katika vizimba umekuwa tishio kwao kiafya na kibiashara hasa katika msimu wa masika hivyo taarifa ya kwamba halmashauri hiyo imepokea kibari kutoka TAMISEMI cha kununua Trekta la kuzolea taka inaweza kumaliza tatizo la kukithiri kwa takataka katika vizimba mjini humo.
Ikumbukwe kwamba kila jumamosi ya mwisho ya mwezi hutumika kufanya usafi wa mazingira nchi nzima ,zikiwa ni jitihada za mh rais za kuifanya Tanzania mpya isiyo na maginjwa yasababishwayo na Uchafu wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment