MABAO 25 YA LUKAKU YA MSIMU 2015/2016 MPAKA MICHUANO ILIPOFIKIA YAMEKUWA LULU


Image result for LUKAKU
Image for the news result
Image result for LUKAKURomelu Lukaku ametoboa waziwazi kutoridhishwa na Klabu yake Everton na kuonyesha nia ya kujiunga na Klabu nyingine ili acheze UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Lukaku, ambae Msimu huu amepachika Mabao 25, yupo kambini na Timu ya Taifa ya Belgium ikijitayarisha kucheza na Portugal Jumanne.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amesema hatua nyingine kwenye Soka lake ni kujiunga na Klabu nyingine ili acheze Mashindano ya Ulaya Msimu ujao kitu ambacho Everton, ambao wapo Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England na Pointi 13 nyuma ya Timu ya 4 Man City hawawezi wakikipata Msimu huu.

Huku Baba yake Mzazi akimhimiza ahamie Klabu kubwa kama Bayern Munich na Manchester United, Lukaku amesema hizo ni Klabu ambazo Baba yake anazipenda lakini Wakala wake yupo kazini ambae anashughulikia masuala yake.

Lukaku amehusishwa pia na kurejea Chelsea ambako aliondoka kwa Dau la Pauni Milioni 28 kuhamia Everton Mwaka 2014 lakini mwenyewe ametamka: “Hapana, nitasema hapana kwa hilo. Sina cha kujiridhisha huko. Nilihama na wao wakasonga. Wakatwaa Ubingwa na mimi nikaongeza ubora na sasa tutazame baadae kuna nini!”

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford              
1700 Bournemouth v Man City    
1700 Norwich v Newcastle          
1700 Stoke v Swansea               
1700 Sunderland v West Brom    
1700 West Ham v Crystal Palace  
1930 Liverpool v Tottenham                 
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton    
1800 Man United v Everton     
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment